NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, amefanikiwa kumaliza mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 10 kati ya vijiji vya Bomalang’ombe na Lyamko wilayani Kilolo, kuhusu mgawanyo wa hisa za Kampuni ya Bomalang’ombe Village Company Limited (BVC) iliyokuwa akizalisha umeme na miradi mbalimbali
Mgogoro huo wa muda mrefu uliathiri shughuli za uzalishaji mali za kampuni hiyo ikiwemo uzalishaji wa nishati ya umeme, na kusababisha hasara kwa pande zote zinazohusika kwa kipindi cha miaka10.
Chanzo cha mgogoro huo kilianzia mwaka 2015, kipindi ambacho Halmashauri ya Iringa na Kilolo zilikuwa bado hazijagawanywa.
Baada ya mgawanyo wa halmashauri, eneo la mradi wa BVC likabaki katika kijiji cha Lyamko ndani ya wilaya ya Kilolo, jambo lililosababisha mivutano ya muda mrefu kuhusu umiliki na mgao wa hisa.
Baada ya kuona hivyo ndipo i Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, ameonyesha uongozi huo kwa kuingilia kati mgogoro ambao kwa miaka mingi umeathiri maendeleo ya wananchi na ucheleweshaji wa mapato kwa vijiji vinavyonufaika na mradi huo.
Kupitia mazungumzo ya pamoja na pande zote, DC Sitta amehakikisha kunapatikana mgawanyo sawa na wa haki wa hisa za kampuni hiyo, hatua inayotarajiwa kufufua shughuli za uzalishaji na kuimarisha mapato ya vijiji vya mradi pamoja na halmashauri husika.
Kampuni ya BVC, ambayo ndiyo chanzo cha mgogoro huo, imekuwa ikijishughulisha na uzalishaji wa nishati ya umeme unaotokana na vyanzo vya maji katika eneo hilo.
Baadhi ya viongozi wa vijiji vya Lyamko na Bomalang’ombe pia wameelezea namna suluhu hiyo itakavyosaidia kuimarisha mahusiano na kuchochea maendeleo katika vijiji hivyo.
DC Sitta aliwapongeza Wakurugenzi na wakuu wa idara ya Iringa Vijijini kwa kuona hilo na kuhakikisha wanamaliza mgogoro huo na kuhakikisha mradi huo wa mfano na historia unaanza rasmi na kuntaka mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na timu nzima kutochelewesha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Iringa Dc, Robert Masunya alisema kuwa kuna miradi zaidi ya minne katika kampuni hiyo ya BVC ambapo mradi mkubwa ni uzalishaji wa umeme , mradi wa ufugaji wa Ng'ombe, Nguruwe na wanyama wengine, mradi wa misitu.
Alisema kuwa kutokana na mgogoro kuisha watakwenda kuzalisha miti na kuongeza ukubwa wa hekari amhapo hadi sasa ziko mia nne , kuendeleza ufugaji ambao kama uikuwa haufanyi kazi.





No comments:
Post a Comment