Na Mbaruku Yusuph,Tanga
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman amesikitishwa na taarifa toka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF) ya kuufungia uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga kwa kukosa vigezo vya kutumika katika michezo ya Ligi Kuu.
Alisema kwa kuwa CCM ndio mmiliki halali wa kiwanja hicho chama hicho kimeamua kufanya ziara katika uwanja huo ili kujionea hali ya uwanja huo ulivyo na kubaini chanzo cha kasoro hizo ambapo uwanja huo umetoka kufanyiwa marekebisho miezi michache iliyopita
Komred Rajabu hakuridhishwa na taarifa toka kwa Meneja wa uwanja huo baada ya kuutembelea uwanja ambapo aliambatana na baadhi ya viongzi wa CCM na kupelekea kutoa maelekezo ya kuundwe kwa kamati ndogo ya Siasa Mkoa,Meneja wa uwanja na TFF ili kuweza kutatua kasoro zilizoainishwa na Shirikisho hilo ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka iwezekanavyo.
"Kiukweli nimesikitishwa sana uwanja unafungiwa huku wapo watu walio pewa dhamana ya kuusimamia na katibu wetu wa ccm Mkoa ndio mtendaji mkuu na mwenye dhamana ya usimamizi wa uwanja huu".
Rajabu ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa hata wale watakaofanya uzembe wajiengue ili wapatikane viongozi watakaokwenda sambamba na kasi ya Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta ya michezo.
Alisema kuwa inawezekana wakati uwanja unafanyiwa ukarabati wataalamu hawakuwa makini hasa kuweka udongo sahihi unaotakiwa,aina ya nyasi kutokana na hali ya hewa ya mkoa n.k na "Sipendi kuamini hicho kinachozungumzwa na msimamizi wa uwanja huo(meneja)"Alisema Komred Rajabu.
Ipo haja sasa kasoro zilizotolewa na TFF zirekebishwe kwa haraka ili kutoa fursa kwa wanasoka Mkoani Tanga,fursa za kibiashara na kuondoa gharama zitakazozikabili timu kucheza ligi kuu nje ya Mkoa wake.
Katibu wa ccm Mkoa Tanga Mfaume Kizigo alikiri ukweli wa hoja Mwenyekiti huyo ya kuhoji madhaifu ya uwanja huo na kupelekea kufungiwa na tff kwa sababu kazi yake ni kusimamia maono ya Mh, Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa ccm Taifa.
"kweli hata sisi tumeshtushwa na taarifa hii ya kufungiwa kwa uwanja huu wa mkwakwani na ipo haja ya kumsikiliza meneja wetu wa uwanja atoe taarifa ya nini kimetokea mpaka uwanja kuwa katika hali hiyo".
Kwa upande wake Meneja wa uwanja huo Akida Juma alisema takriban siku saba nyuna uwanja ulikuwa na hali nzuri ila ulizungukwa na wadudu aina ya mchwa na tukaamua kupiga dawa jambo baya zaidi hakukuwa na maji kati tenki zote hapo uwanjani jambo lililopelekea siku mbili uwanja kukosa kumwagiliwa.
Naye Katibu wa timu ya Coastal Union inayoshiriki ligi Kuu Omari Ayubu alisema wameshawasiliana na wamiliki wa uwanja huo ambao ni ccm na kama kama Coastal watahakikisha uwanja huo unakuwa katika hali nzuri.
Ayubu alisema swala la kutafuta uwanja kwa michezo yao ya ligi Kuu matarajio yao kushirikiana na wamiliki wa wauwanja ili kuhakikisha uwanja unarudi katika ubora wake ili waweze kuutumia katika mechi zao za ligi kuu y NBC.
"Tunatarajia kufanya juu chini tubakibkatika uwanja wetu wa Mkwakwani itakapotubidi kuondoka basi tutatangaza uwanja gani tutautumia wakati uwanja huu ukiendelea na marekebisho"Alisema Omari Ayubu.

.jpg)
.jpg)
.jpg)


No comments:
Post a Comment