Na Mbaruku Yusuph,Tanga
SHIRIKA la Nyumba la Taifa(NHC)Mkoani Tanga limeanzisha mradi wa Jengo la kisasa la kibiashara litakalokuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Bil 8.4. hatua hiyo imekuja baada ya kufunguka kwa fursa za kiuchumi Mkoani hapa.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika hilo Mkoani hapa Mhandisi Mussa Kamendu alipozungumza na mwandishi wa Habari mseto ofisini kwake nakuongeza kuwa jengo hilo litakuwa na ghorofa saba na mandhari nazuri ya maegesho ya magari.
Mhandisi Kamendu alisema Mkoa wa Tanga unakuwa kutokana na ongezeko la fursa za kiuchumi kama mradi wa bomba la mafuta,maboresho ya Bandari ya Tanga,zao la Mkonge na viwanda na kupelekea mkoa huu kuwa na ongezeko la wageni toka ndani na nje ya nchi ambao wanauhitaji wa ofisi na makazi.
"tupo tayari kuitumia fursa hii ya ukuaji wa uchumi Mkoani hapa na ndio maana sisi kama NHC tumeanza na jengo la kisasa la kibiashara"Alisema Mhandis Kamendu.
Aidha katika taarifa yake alisema mbali ya mradi huo Shirika hilo linatarajia kujenga miradi mengine mikubwa sambamba na kuzifanyia marekebisho nyumba zinazomilikiwa na Shirika hilo ili kukidhi matakwa ya ongezeko la wateja wanaohitaji nyumba za kuishi pamoja na ofisi.
Mhandisi Kamendu alifafanua zaidi na kusema kuwa jengo hilo linajengwa katika eneo la Mkwakwani na ndio sababu ya kuitwa Mkwakwani Plaza ambapo ghorofa tatu za chini zitakuwa za biashara na ofisi mbalimbali na ghorofa nne za juu kutakuwa na nyumba ishirini za makazi ya watu.
"Jengo hili litakuwa la kisasa zaidi ambapo katika ghorofa nne za juu kutakuwa na nyumba kumi zenye vyumba viwili viwili na nyumba kumi zenye vyumba vitatu vitstu na zaidi tunazingatia sana kuweka mifumo mizuri ya kiusalama,maji safi, taka, n.k' Alisema Mhandi Kamendu.
Kwa upande wake Msimamizi msaidizi wa ujenzi mradi huo Mhandisi John Mchechu alisema mradi huo upo katika asilimia 16 ambapo utekelezaji wake ulianza mwezi June mwaka 2025 na unatarajia kukamilika mwezi June mwaka 2027.
Mhandisi Mchechu alisema matarajio kuumaliza mradi huo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wananchi waweze kulitumia jengo hilo kama ilivyokusudiwa na Shirika hilo.





No comments:
Post a Comment