Kikosi Kazi cha dharura katika Hospital ya Dk. Ole Lengine kikionesha kazi zake ndani ya gari la kusaidia wagonjwa wa dharura.
Mkurugenzi wa Hospital ya Dk. Ole Bi Bertha Emmanuel akipewa mkono wa pongezi na Mtendaji kutoka manispaa ya Ubungo DK. Felister Kimolo, hii ni katika kuunga mkono ushirikiano wa huduma za afya kati ya serikali na sekta binafsi.
NA ASHA BANI
HOSPITAL I ya Dk. Ole Lengine Memorial imeongeza gari mpya na ya kisasa ya kisasa ya huduma ya dharura (Ambulance).
Mkurugenzi wa Hospital hiyo, Bertha Emanuel alisema wanayofuraha kuongeza gari hilo kwani inasaidia katika kuongeza ufanisi na huduma ya dharura kwa wagonjwa.
"Tunafuraha kwani kuongeza gari hilo ya huduma ya dharura inasaidia kwa wagonjwa wa eneo hilo wa maeneo ya jirani,"alisema Bertha.
Mgeni rasmi katika hafla ya makabidhiao hayo ni Mchungaji Ezekiel Ngao aliyeambatana na mwakilishi wa ofisi ya DMO Dk. Felister Kimolu ambapo kwa nyakati tofauti walipongeza hatua ya uongozi wa hospital hiyo ambayo inawasaidia wananchi kupata huduma nzuri ya haraka zaidi.

.jpeg)

No comments:
Post a Comment