HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

May 12, 2026

JAMII MKOANI KAGERA YATAKIWA KULINDA NA KUTUNZA ARDHI KUEPUKA MMOMONYOKO

NA EDITHA WILLIAM, KAGERA


Jamii Mkoani Kagera imetakiwa kulinda na kutunza ardhi ili kuepuka mmomonyoko wa ardhi ikiwa ni sambamba na kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu juu ya matumizi sahihi ya eneo husika.


Hayo yamezungumzwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kagera Erick Peter Makundi alipokuwa ofisini kwake wakati akielezea mabadiliko ya tabia ya nchi na athari za  matumizi ya ardhi  ndani ya Mkoa wa Kagera  


Aidha makundi ameongeza kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi makubwa ambayo yameononekana ndani ya mkoa wa kagera ni pamoja na mvua nyingi ambazo zimeathiri maeneo mbali mbali na makazi ya watu wanapoishi kila siku na  kuongezeka kwa joto.


vile vile amesema kuwa matumizi ya ardhi yanapangwa kutokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na standadi zinazowekwa mfano majengo ya makazi , barabara na  majengo ya kuabudia 


" Wizara ya Ardhi  tunashirikiana na wizara mbalimbali hapa mkoa wa kagera hasa wizara ya mazingira,   kuhakikisha mazingira yetu yanaborehwa ili kupambana na suala la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa mfano kwenye hati zetu tumejiwekea sharti kwamba mtu anapohitaji  hati  ya kumilikishwa ardhi lazima ahakikishe amepanda miti isiyopungua kumi."


Hata hivyo, amesema kuwa jamii imekuwa ikishirkishwa katika mipango yote ya matumizi ya ardhi {mipango kina} ambapo zoezi hilo limekuwa likiendelea ndani ya mkoa wa kagera na  nchini nzima kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Pages