Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo
amehudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, zilizofanyika jijini Kampala, Uganda.
Rais Museveni ameapishwa kuiongoza Uganda kwa muhula mwingine baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 15 Januari, 2026.
Ushiriki wa Rais Dkt. Samia ni kielelezo cha kuendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Uganda, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda, kwa maslahi ya pamoja ya wananchi wa pande zote mbili.
Tanzania na Uganda ni washirika wa karibu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiendelea kuimarisha ushirikiano katika nyanja za diplomasia, biashara, uwekezaji, nishati, uchukuzi, miundombinu, kilimo, viwanda, uhamiaji na miradi ya kimkakati ya kikanda.
Katika biashara, nchi hizo zimeendelea kuboresha mifumo ya uwezeshaji biashara,uongezaji wa thamani za bidhaa na kushirikiana katika kutatua changamoto zilizopoikiwemo vikwazo visivyo vya kikodi. Hatua hii inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma ndani ya ukanda kupitia ushoroba wa kati.





No comments:
Post a Comment