HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 05, 2026

CRDB Yatenga Bilioni 2 Kuongeza Matumizi ya SimBanking


Meneja wa Huduma ya Kibenki kupitia simu za mkononi wa Benki ya CRDB, Amina Mawona (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi mbalimbali kampeni ya SimBanking Kimpango Wako jijini Dar es Salaamm leo kulia ni meneja mahusianohuduma za kibenki kidigitali, Richard Ochaka, na kushoto ni Meneja Uhifadhi na Biashara ya Wakala wa benki hiyo, Erasto Alfred, na balozi wa kampeni hiyo, Juma Ayo.


Na Mwandishi Wetu


BENKI ya CRDB imetenga jumla ya Shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kampeni ya SimBanking Kimpango Wako, inayolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kidijitali na kuongeza idadi ya wateja wanaofanya miamala kupitia SimBanking.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Huduma za Kibenki Kupitia Simu ya Mkononi wa CRDB, Amina Mawona, amesema kampeni hiyo itaendelea hadi mwisho wa mwaka ikiwa na zawadi mbalimbali kwa wateja wanaotumia SimBanking kufanya miamala.



Amesema pamoja na zawadi za kila mwezi, kampeni hiyo itahitimishwa kwa droo kubwa ambapo mshindi wa kwanza atajishindia Shilingi milioni 30, mshindi wa pili milioni 20 na mshindi wa tatu milioni 10.

Mawona amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma za kifedha kidijitali ambazo ni salama, rahisi na zenye kuokoa muda, huku wafanyabiashara wakihimizwa kutumia huduma za Lipa Namba zinazofanya kazi kwenye mitandao yote ya simu.


Awali, Meneja Mahusiano wa Huduma za Kibenki Kidijitali wa CRDB, Richard Ochaka, alisema benki imeendesha droo ya nne ya mwezi ya kampeni hiyo na kupata washindi 116.

Alisema washindi 100 wamejishindia Shilingi 50,000 kila mmoja, washindi 11 wamepata simu janja na wanafunzi watano wenye akaunti za Scholar wamejishindia laptop za kisasa.



Ochaka aliongeza kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo, zaidi ya washindi 2,000 wamenufaika na zawadi mbalimbali, huku droo zikiendelea kufanyika kila mwezi hadi mwisho wa mwaka.

No comments:

Post a Comment

Pages