October 27, 2026

Waziri Kapinga azindua kiwanda cha Simba Beverages

Na Mwandishi Wetu, Kibaha


Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amezindua kiwanda cha vinywaji baridi cha Simba Beverages Limited kilichopo Chekereni Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kapinga alisema uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya Simba Beverages ni kielelezo cha ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Katika hotuba yake Kapinga alinukuu maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba pamoja na uwepo wa Viwanda lakini anapendezwa na viwanda vipya na kueleza kuwa ndio maana serikali hailali usingizi. Kapinga alisema mwaka huu 2026 vimejengwa viwanda vikubwa 25 huku 20 vikifanya kazi.


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Nkurlu alisema kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2021 hadi 2022 viwanda 1387 vimejengwa na kufikia Septemba 2026 vimejengwa viwanda 1768. Nkurlu alisema viwanda 99 vingine vinajengwa.


Alisema mkoa wa Pwani lenye ukubwa wa Hekta 148000 likiwa na kongani 35. Mkurugenzi wa TanTrade, Ephraim Mafuru alisema uwekezaji uliofanywa na Simba Beverages ni mchango mkubwa wa Pato la Taifa.


Mafuru alitoa wito kwa wawekezaji ili waweze kutambulika watumie nembo ya uzalishaji ya Tanzania. Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na utetezi wa TPSF Mwanahamis Hussein alipongeza hatua hiyo ya uwekezaji kwa sababu imeongeza soko la ajira na kuleta ushindani wa kiuchumi.


Hussein pia aliupongeza mkoa wa Pwani kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. Mkuu wa Masoko wa Simba Beverages Limited Spandan Ray alisema wamejipanga kuwekeza zaidi katika nyanja ya viwanda.

No comments:

Post a Comment

Pages

▼