Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amezindua kiwanda cha vinywaji baridi cha Simba Beverages Limited kilichopo Chekereni Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kapinga alisema uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya Simba Beverages ni kielelezo cha ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhili Nkurlu alisema kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2021 hadi 2022 viwanda 1387 vimejengwa na kufikia Septemba 2026 vimejengwa viwanda 1768. Nkurlu alisema viwanda 99 vingine vinajengwa.
Alisema mkoa wa Pwani lenye ukubwa wa Hekta 148000 likiwa na kongani 35. Mkurugenzi wa TanTrade, Ephraim Mafuru alisema uwekezaji uliofanywa na Simba Beverages ni mchango mkubwa wa Pato la Taifa.
Mafuru alitoa wito kwa wawekezaji ili waweze kutambulika watumie nembo ya uzalishaji ya Tanzania. Mkurugenzi wa Sera, Utafiti na utetezi wa TPSF Mwanahamis Hussein alipongeza hatua hiyo ya uwekezaji kwa sababu imeongeza soko la ajira na kuleta ushindani wa kiuchumi.
Hussein pia aliupongeza mkoa wa Pwani kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. Mkuu wa Masoko wa Simba Beverages Limited Spandan Ray alisema wamejipanga kuwekeza zaidi katika nyanja ya viwanda.





No comments:
Post a Comment