December 31, 2012

VIDEO YA WIMBO WA BODABODA YAKAMILIKA


Na Elizabeth John

HATIMAYE video ya wimbo wa ‘Bodaboda’ ulioimbwa na wakali wa muziki wa bongo fleva nchini, Ismal Seif ‘Suma Lee’ na Sunday Mangu ‘Linex’ imekamilika na tayari imesambazwa katika vituo mbalimbali vya televisheni.

Bodaboda ni wimbo ambao umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio ambapo baadhi ya washabiki waliwashauri wasanii hao wafanye haraka kutengeneza video ya wimbo huo ili waone kinachozungumziwa ndani ya wimbo huo.

Akizungumzia kazi hiyo, Linex alisema kazi hiyo imekamilika na tayari imeshaanza kuonekan akatika vituo mbalimbali vya luninga anaomba mashabiki wao wawape sapoti katika wimbo huo.

“Kazi hii tumefanyia hapa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo tulishuti tukiwa visiwani Zanzibar, naamini itakua vizuri maana haikuwa kazi ya kitoto tunaomba tu mashabiki wetu watupe sapoti ya kutosha katika kazii ambayo imetengenezwa kwa maadili ya Kitanzania,” alisema Linex.

Linex ni msanii ambaye anafanya vizuri katika muziki huo, anatamba na vibao vyake vingi kikiwemo ‘Aifola’ anachotamba nacho sasa na ‘Hakunaga’ ni kibao cha Suma Lee ambacho kilitamba zaidi, licha ya kuwa na vibao vingi ambavyo amevifanya.

No comments:

Post a Comment

Pages