January 01, 2013

DE GEA, LUIS NANI KUMBADILI CRISTIANO RONALDO


Cristiano Ronaldo

MADRID, Hispania

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji Cristiano Ronaldo hawezi kuigharimu Manchester United kiasi cha pauni milioni 122, kama ataamua kuihama klabu yake ya Real Madrid.

Kama Ronaldo atahitaji kuihama klabu hiyo ya Santiago Bernabeu kama alivyosema wiki iliyopita, ni wazi kuwa Real itapaswa kushusha kwa kiasi kikubwa thamani ya mchezji, ili kuruhusu pia mazungumzo na nyota kadhaa.

Punguzo hilo linaweza kushuka na kufikia pauni milioni 60 pamoja na David de Gea, huku pia kukiwa na uwezekano wa kiungo Mreno wa United, Luis Nani kujiunga na Madrid.

SunSport imefichua habari mpya kwamba Ronaldo amewathibitishia baadhi ya marafiki zake wa zamani wa klabu ya Manchester United, kuwa angependa kurejea nyumbani Old Trafford.

Mchambuzi na mwandishi wa michezo wa The Sun wiki jana alielezea namna kulivyo na uwezekano wa Ronaldo kulazimisha kuihama Madrid na kurejea Manchester, wakati huu ambapo amebakisha miaka miwili ya mkataba wake wa sasa. 

Katikati ya wiki, gazeti la kila siku jijini hapa la AS, lilifichua kwamba Ronaldo hana mpango wa kuboresha mkataba wake na Real Madrid.

Chanzo cha habari hiyo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Ronaldo, ambaye alikubali kusaini karatasi ya tamko hilo iliyonaswa na gazeti hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages