December 31, 2012

WALTER AWAHAIDI MAKUBWA WATANZANIA



Na Elizabeth John

MSHINDI wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) mwaka jana, Walter Chilambo amesema Watanzani wategemee vutu vizuri kutoka kwake kwamba yeye ni msanii mwenye kipaji na hakupata ushindi huo kwa kubahatisha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Walter alisema wasanii wengi ambao wanashinda BSS huwa wanapotea na hawaonekani tena katika soko la muziki yeye anakujua kivingine anaomba mashabiki wa muziki wakae mkao wa kula.

“Washindi wengi wa BSS wanaishia hewani, mimi naamini nitakua tofauti sana kwani nimejipanga kuleta mabadiliko ya muziki kwa vijana wa Tanzania kwa kupitia BSS,” alisema Walter.

Walter alisema kwasasa yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Siachi’  ambapo Jumatatu anatarajia kuutambulisha  na kuusambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

Mbali na kibao hicho Walter yupo kwenye maandalizi ya kuachia albamu yake ya kwanza ambayo bado hajaipatia jina, itakua na nyimbo zaidi ya kumi.

“Naomba mashabiki wa bongo fleva wakae mkao wa kula, wimbo wangu wa kwanza nitautambulisha Jumatatu na albamu itakua tayari mwishoni mwa mwezi huu tuombe uzima kutoka kwa mwenyezi mungu ili wapenzi wangu mpate burudani iliyoenda shule,” alisema Walter.

No comments:

Post a Comment

Pages