January 19, 2013

DARREN FLETCHER NJE MSIMU MZIMA MAN UTD

MACHESTER, England

‘Darren Fletcher hatoweza kupatikana dimbani katika kipindi kilichosalia msimu huu, baada ya kufanyiwa upasuaji kumaliza tatizo sugu la tumbo lake’

MANCHESTER United imethibitisha rasmi kuwa kiungo wake nyota Darren Fletcher atakuwa nje ya dimba hadi mwishoni mwa msimu huu kutokana na upasuaji wa tatizo sugu la uvimbe wa tumbo.

Fletcher, 28, nyota wa kimataifa wa Scotland, amedumu na taizo hilo na kupigana nalo kwa miaka miwili sasa na Man United inadhani ili kuondoa shaka ya mkali huyo katika mustakabali wake wa soka – ililazimu kukubali upasuaji huo.

Nyota huyo alionekana kwa mara ya mwisho dimbani alipoingia kama mtokea benchi katika ushindi wa United wa mabao 4-3 dhidi ya Newcastle Desemba 26 ‘Boxing Day’, na amecheza wastani wa mechi 10 tu msimu huu tangu aliporejea toa majeruhi Septemba.

‘Darren Fletcher hatoweza kupatikana dimbani katika kipindi kilichosalia msimu huu, baada ya kufanyiwa upasuaji kumaliza tatizo sugu la tumbo lake,’ ilisema taarifa ya United kupitia tivuti yake.

‘Upasuaji huu ni utaratibu uliokuwa umepangwa kufanywa katika kipindi hiki cha mafanikio ya hali yake, uthibitisho wa maendeleo yake mazuri ni kujumuika kwake kwa mazoezi na kupangwa mara kwa mara msimu huu hadi operesheni yake.

‘Mengi tumeyazingatia sisi kama timu, lakini yeye pia na familia yake kwa ajili ya maajaliwa ya soka lake la baadaye. Uamuzi huu umezingatia hilo na tuko tayari kuona mafanikio na klabu ina matumaini makubwa na marejeo yake msimu ujao,’ ilieelza taarifa hiyo.

……..Daily Mail……….

No comments:

Post a Comment

Pages