January 01, 2013

PETER NDLOVU ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI

Peter Ndlovu (katikati waliokaa) akiwa katika kiti maalum cha wagonjwa kwenye Hospitali ya Mater Dei jijini Bulawayo alikokuwa amelazwa.

HARARE, Zimbabwe

Kwa mujibu wa kaka mkubwa wa familia yao, Madinda Ndlovu, hali ya nduguye ilikuwa imeimarika sana kwa sasa. Alisema wakati Peter akiruhusiwa, alimudu kutabasamu na kuzungumza machache na watu waliokuja kumtembelea

NAHODHA wa zamani wa klabu ya Warriors, Peter Ndlovu ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Mater Dei jiji Bulawayo alikokuwa anatibiwa.

Nyota huyo wa zanmani wa Coventry City ya England, ambaye ni miongoni mwa wachezaji maarufu waliopata kung’ara nje ya hapa Zimbabwe, alilazwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali mbaya iliyochukua uhai wa kaka yake Adam.

Kwa mujibu wa kaka mkubwa wa familia yao, Madinda Ndlovu, hali ya nduguye ilikuwa imeimarika sana kwa sasa. Alisema wakati Peter akiruhusiwa, alimudu kutabasamu na kuzungumza machache na watu waliokuja kumtembelea.

Familia ya Ndlovu kwa sasa inatafakari kumpeleka ndugu yao huyo Peter nchini England kupata matibabu zaidi: “Nadhani ni ni vizuri kuwa naye nyumbani,” alisema Madinda kumzungumzia Peter.

“Na kama nilivyosema hapo awali, kuwa tunafikiria kumsafirisha kwa ndege kwenda England kwa matibabu zaidi.

“Tunawashukuru wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijitoa kutusaidia familia katika kipindi hiki kigumu cha hali ya ndugu yetu na msiba wa ndugu mwingine.

“Kwa sasa sisi tunaelekeza nguvu zetu katika kuhakikisha kwamba hali ya Peter inatengemaa na kumrudisha katika haali yake ya kawaida.”

Nyota huyo aliyewahui kuichezea Mamelodi Sundowns, alivuta hisia za wengi akiwa hospitalini amelazwa, ambapo alitembelea na watua kadhaa maarufu akiwamo Mwanasiasa Obert Mpofu, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Madini wa Serikali ya Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Pages