January 20, 2013

DOMO LANGU KUBEBA JINA LA ALBAMU YA TIMBULO


Na Elizabeth John

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo ‘Timbulo’ anajipanga kuachia albamu yake ya kwanza inayokwennda kwa jina la ‘Domo langu’ ambayo itakua na jumla ya nyimbo kumi.

Timbulo alishawahi kutamba na vibao vyake kama Domo langu ambacho kimebeba jina la albamu hiyo, Timbulo wa leo, Samson na Delila na vinginevyo ambavyo vinanfanya vizuri katika soko la muziki wa kizazi kipya. 

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Timbulo alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa albamu hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri katika soko la muziki hilo kutokana na nyimbo zilizobeba albamu hiyo.

“Namshuku mungu asilimia kubwa ya kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu hivyo ninaimani hata kazi hii itapokelewa vizuri kwani nyimbo zilizomo humo ni moto wa kuotea mbali,” alisema Timbulo.

Alisema kwasasa anajianndaa kukamilisha kazi yake ambayo nayo itakuwepo ndani ya albamu hiyo, inayokwenda kwa jina la ‘Lastiki ya upendo’ ambayo amewashirikisha wasanii wa kundi la Malea kutoka Cameroon.

Msanii huyo kwasasa anatamba na ngoma yake ya ‘Bado kijana’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga kutokana na ujumbe uliobeba.

No comments:

Post a Comment

Pages