January 20, 2013

TUNDAMAN AKAMILISHA KALENDA YA 2013


Na Elizabeth John

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ amesema amekamilisha kalenda yake ya mwaka 2013 ambayo itamuwezesha kufanya kazi zake katika mpangilio mzuri.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Tunda alisema kila anapoingia mwaka mpya huwa anatabia ya kupanga ratiba ya mwaka mzima kwa lengo la kufanya kazi zake katika mpangilio mzuri.

“Unajua hii inasaidia kufanya kazi zako vizuri kutokana na kujua siku gani unafanya nini, kwahiyo unajipanga kwaajili ya siku hiyo mimi naamini nikiwa najua siku Fulani naenda kufanya shoo sehemu lazima nitajiandaa na kufanya mazoezi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuchagua nyimbo ambazo najua nikiziimba nitawafurahisha mashabiki wangu na sio kukurupuka  tu,” alisema Tunda Man.

Alisema anawaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kupokea vitu vizuri kutoka kwake, na kwamba anajipanga kuachia kazi yake mpya ambayo hajataka kuitaja jina kutokana wizi uliopo hadharani kati ya wasanii wenyewe pamoja na waharamia katika tasnia ya muziki huo.

Tunda Man anatamba na kibao chake cha ‘Demu sio’ mbali na kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

No comments:

Post a Comment

Pages