Frank Lampard akishangilia moja ya mabao yake mawili aliyofunga na kuipa Chelsea ushindi wa mabao 2-1
Shabiki akionesha bango la kumuomba mmiliki wa Chelsea kutomuacha kiungo Frank Lampard
LONDON, England
"Hatujazungumza lolote
juu ya mkataba mpya na klabu katika wiki za karibuni. Kwa wakati huu hakuna
kinachosemwa kuhusu hilo
na mkataba wangu unafikia tamati kiangazi kijacho na hili linajulikana ndani na
nje ya klabu"
KIUNGO wa Chelsea, Frank
Lampard amesema hakuna mchakato wowote wa nyongeza ya mkataba wake na klabu
hiyo ya Stamford Bridge, licha ya kiwango cha juu
anachoonesha katika siku za karibuni.
Lampard, 34, nyota wa
kimatauifa wa England,
ambaye mkataba wake wa sasa unafikia tamati kiangazi kijacho, yuko huru kuingia
mkataba wa awali na klabu yoyote ya nje katika kipindi hiki hiki cha usajili wa
majira ya baridi unaonza leo barani Ulaya.
"Hatujazungumza lolote
juu ya mkataba mpya na klabu katika wiki za karibuni," alisema Lampard ambaye
alifunga mabao yote mawili ya Chelsea
katika ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Everton, Jumapili.
"Kwa wakati huu hakuna kinachosemwa
kuhusu hilo na
mkataba wangu unafikia tamati kiangazi kijacho na hili linajulikana ndani na
nje ya klabu."
Mabao mawili ya Lampard katika
ushindi wa Blues huko Goodison
Park, ina maana kuwa
mkali huyo yuko nyuma kwa bao moja dhidi ya Kerry Dixon aliyefunga mabao 193 na
kushikilia rekodi ya klabu hiyo ya mfungaji wa muda wote, ambayo inaongozwa na Bobby
Tambling aliyefunga mabao 202.
Baada ya kuanza kwa kuwekwa
benchi na kocha wa sasa Rafael Benitez, Lampard ameonesha zinduko la aina yake
akicheza na kufunga kwa kiwango cha juu – akifunga katika mfululizo katika
mechi tatu zaa Ligi Kuu zilizopita alizoanza kikosi cha kwanza.
Lampard amesisitiza kuwa ana
furaha kuwa sehemu ya timu hiyo iliyocheza na kushinda mechi nne mfululizo za
Ligi Kuu chini ya Benitez.
"Nina furaha mno kucheza,
nafanya kazi ngumu, kwa bidii mazoezini, ninapenda kuwa sehemu ya timu hii,"
aliongeza Lampard.
"Yote kwa yote naweza
kukwambai kwamba ni jambo jema na nina furaha kwamba naendelea kucheza vema
kikosini kama nilivyoonesha leo katika mechi
hii," alimaliza Lampard ambaye anawindwa na LA Galaxy kujaza pengo la
David Beckham.
No comments:
Post a Comment