Peter Ndlovu (katikati waliokaa) akiwa katika kiti maalum cha wagonjwa kwenye Hospitali ya Mater Dei jijini Bulawayo alikokuwa amelazwa.
HARARE, Zimbabwe
Kwa mujibu wa kaka mkubwa wa familia yao, Madinda
Ndlovu, hali ya nduguye ilikuwa imeimarika sana kwa sasa. Alisema wakati Peter akiruhusiwa,
alimudu kutabasamu na kuzungumza machache na watu waliokuja kumtembelea
NAHODHA wa zamani wa klabu ya Warriors,
Peter Ndlovu ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Mater Dei jiji Bulawayo alikokuwa anatibiwa.
Nyota huyo wa zanmani wa Coventry City
ya England, ambaye ni
miongoni mwa wachezaji maarufu waliopata kung’ara nje ya hapa Zimbabwe, alilazwa hospitalini hapo
baada ya kupata ajali mbaya iliyochukua uhai wa kaka yake Adam.
Kwa mujibu wa kaka mkubwa wa
familia yao, Madinda Ndlovu, hali ya nduguye
ilikuwa imeimarika sana
kwa sasa. Alisema wakati Peter akiruhusiwa, alimudu kutabasamu na kuzungumza
machache na watu waliokuja kumtembelea.
Familia ya Ndlovu kwa sasa
inatafakari kumpeleka ndugu yao huyo Peter nchini
England
kupata matibabu zaidi: “Nadhani ni ni vizuri kuwa naye nyumbani,” alisema Madinda
kumzungumzia Peter.
“Na kama nilivyosema hapo
awali, kuwa tunafikiria kumsafirisha kwa ndege kwenda England kwa
matibabu zaidi.
“Tunawashukuru wote ambao kwa
namna moja ama nyingine walijitoa kutusaidia familia katika kipindi hiki kigumu
cha hali ya ndugu yetu na msiba wa ndugu mwingine.
“Kwa sasa sisi tunaelekeza
nguvu zetu katika kuhakikisha kwamba hali ya Peter inatengemaa na kumrudisha
katika haali yake ya kawaida.”
Nyota huyo aliyewahui
kuichezea Mamelodi Sundowns, alivuta hisia za wengi akiwa hospitalini amelazwa,
ambapo alitembelea na watua kadhaa maarufu akiwamo Mwanasiasa Obert Mpofu, ambaye
kwa sasa ni Waziri wa Madini wa Serikali ya Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment