Radamel Falcao akishangilia kufunga mabao matatu 'hat-trick' katika moja ya mechi zake akiwa na Atletico Madrid
MADRID, Hispania
“Najivunia sana kuona idadi
kubwa ya klabu zikionesha kunihitaji, lakini zitalazimika kusubiri hadi
mwishoni mwa msimu huu. Kisha tutaona nini kitatokea juu yangu. Siwezi kuhama Madrid Januari hii”
MSHAMBULIAJI anayepigiwa
hesabu na klabu nyingi zaidi barani Ulaya kwa sasa, Radamel Falcao, amezitaka Chelsea na Manchester
City kusahahu kupata
saini yake katika usajili wa dirisha dogo unaonaza leo Januari 1 barani Ulaya.
Falcao nyota wa kimataifa wa Colombia anayechezea klabu ya Atletico Madrid, amesema hawezi
kuihama klabu yake katika usajili huu, kauli inayozikata maini klabu kadhaa
zinazosaka saini yake, huku akitajwa kakma mmoja wa washambuliaji bora zaidi
duniani.
Licha ya kuwamo kwa kipengele
kinachomruhusu kuihama klabu hiyo kwa dau nono la pauni milioni 47, Falcao
amesema hata kama ikitokea klabu ya kuulizia
uhamisho wake Januari hii hayuko tayari kutoma jijini hapa anakoheshimika.
Falcao, 26, alisema: “Najivunia
sana kuona
idadi kubwa ya klabu zikionesha kunihitaji, lakini zitalazimika kusubiri hadi
mwishoni mwa msimu huu. Kisha tutaona nini kitatokea juu yangu.
“Kuondoka Atletico katika
usajili wa majira ya baridi ni wazi si kati ya mambo yanayoweza kutokea. Nataka
kusaidia mafanikio ya klabu yangu nami kuwa sehemu ya watimizaji malengo.”
Mkali huyu amekuwa katka rada
za muda mrefu za Chelsea, na ilikuwa nusura atue
Stamford Bridge
katika siku ya mwisho ya usajili wa majira ya baridi msimu uliopita.
Mabao yake matatu ‘hat-trick’
katika kuwania UEFA Super Cup, wakati Atletico ikiichapa Chelsea mabao 4-1, yalikuwa
na mchango mkubwa wa kutibua kibarua cha Roberto Di Matteo, huku akikoleza moto
wa kuwindwa na The Blues.
No comments:
Post a Comment