January 01, 2013

LINNAH KUTAMBULISHA NAJIANDAA


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Estelinah Sanga ‘Linnah’ anajipanga kutambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Najiandaa’.

Akizungumzia kazi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Linnah alisema kibao hicho tayari amekikamilisha anachosubiri ni kukisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

Alisema anaomba mashabiki wa kazi zake waendelee kumpa sapoti katika kazi ambazo zinakuja kwani bado kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.

“Naomba mashabiki wangu wasichoke kunipa sapoti katika kazi zangu, nashukuru kwa sapoti waliyonipa kwani inanitia nguvu ya kuendelea kufanya kazi, hivyo naomba wasinichoke katika hili,” alisema Linnah.

Linnah alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Bora nikimbie, Ushanikumbuka, Fitina na nyinginezo ambazo zilifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni

No comments:

Post a Comment

Pages