January 10, 2013

UZINDUZI WA SKULI MPYA YA MADUNGU CHAKE CHAKE PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono wanafunzi wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Madungu Pemba,baada ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Madungu,Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,kuzungumza na wananchi pamoja na wanafunzi hao,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)
 Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi baada ya kuifungua Skuli ya Sekondari ya Madungu Wilaya Chake chake Pemba jana,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Madungu katika Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akilipokuwa akitoa hutuba yake baada ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Madungu,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ili azungumze na wananchi pamoja na Wanafunzi katika kusherehekea ufunguzi wa Skuli Mpya ya Sekondari ya Madungu Wilaya ya Chake chake Pemba,ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo.(Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na Wananchi na wanafunzi wa baada ya kuifungua Skuli Mpya ya Sekondari ya Madungu Wilaya ya Chake chake Pemba,ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages