January 15, 2013

ROBERTO MANCINI, ARSENE WENGER WALIA NA MWAMUZI

Tukio lililomponza nahodha wa Man City Vicente  Kompany kulia na kulimwa kadi nyekundu na kulalamikiwa na kocha Roberto Mancini ndio hili, dhidi ya Jack Wilshere wa Arsenal.

LONDON, England

“Haikuwa rafu kabisa, kwa sababu hatuwezi kupoteza mchezaji wetu muhimu kwa mechi tatu mfululizo bure hivi hivi bila sababu. Ni wazi kwamba haikustahili kuwa kadi nyekundu, tunajiandaa kuikatia rufaa”

MAKOCHA wa klabu Manchester City, Roberto Mancini na wa Arsenal, Arsene Wenger, wameonesha hasira zao kwa kadi nyekundu za moja kwa moja waalizooneshwa mabeki wao Vincent Kompany na  Laurent Koscielny wakati klabu zao zilipoumana juzi.

Mancini bosi wa mabingwa wa soka England, ameipinga vikali kadi ya mwamuzi Mike Dean kwa nahodha wake Kompany, anayodaiwa kupta kutokanana rafu kwa kiungo wa Gunners, Jack Wilshere, huku akisema klabu inajiandaa kuikatia rufaa.

“Haikuwa rafu kabisa, kwa sababu hatuwezi kupoteza mchezaji wetu muhimu kwa mechi tatu mfululizo bure hivi hivi bila sababu. Ni wazi kwamba haikustahili kuwa kadi nyekundu.

“Kompany aliingia akiwania mpira, ingetegemea kama mpinzani angewahi kuuchukua mpira kabla. Sijui inawezekanaje kwa mchezaji kuambulia kadi nyekundu ya moja kwa moja kama hii aliyopewa nahodha wangu,” alisisitiza Mancini.

Kompany alioneshwa kadi nyekundu hiyo na mwamuzi Dean, katika dakika ya 75 ya pambano hilo la Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Emirates, lililoisha kwa Gunners kulala nyumbani kwa mabao 2-0.

Mapema katika pambano hilo, beki Mfaransa wa Arsenal, Koscielny alitolewa nje ya dimba kwa kadi nyekundu, baada ya kufanya madhambi kwa kumzuia isivyo halali mshambuliaji Edin Dzeko asifunge bao.

Wenger aligeuka mbogo na kuilalamikia kadi hiyo, akisema: “Ilinishangaza sana kusema ukweli. Kwa hakika. Nilikataa kuangalia tena marudio ya tukio lile kwa sababu ni kwa kiasi gani limetusaidia hivi sasa?

“Tunaishia kwa kufuata maamuzi ya marefa na kufanya mengi zaidi ya hayo. Nasikia ilikuwa ni penati hatimaye kwa maamuzi ya refa. Ilikuwa kadi nyekundu, Sijui chochote juu ya hilo.”

Kutokana na kadi nyekundu ya Kompany, inamaanisha nahodha huyo atalazimika kukaa jukwaani wakati wa mechi mbili za Man City za Ligi Kuu dhidi ya Fulham na QPR, pamoja na mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA, dhidi ya Crystal Palace au Stoke.

No comments:

Post a Comment

Pages