January 08, 2013

YAYA TOURE AREJEA MAZOEZINI NA TEMBO WA IVORY COAST


Yaya Toure

ABU DHABI, Falme za Kiarabu

MCHEZAJI Bora wa Mwaka 2012 wa Afrika, Yaya Toure amerejea rasmi mazoezini na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ‘Elephants' huko Abu Dhabi, baada ya kukosekana kwa siku mbili kutokana na homa.

Elephant wako huko kujiandaa na fainali za Mataifa Afrika 2013 zinazotarajia kuanza hapo Januari 19, ambpo alilazimika kukosa mazoezi kwa siku mbili na kuzua shaka ya kutowweza kuwa sehemu ya kikosi katika mashindano hayo.

Kaka na nyota mwenzake wa klabu ya Manchester City ya England, Kolo Toure, ambaye pia yupo na kikosi cha Ivory Coast, amepata ruhusa maalum kutoka kwa jopo la madaktari, baada ya kuzuia kufanya mazoezi na wenzake.

"Yaya alikuwa nje ya mazoezi kwa siku kadhaa," Kolo aliiambia tovuti rasmi ya klabu yao na kuongeza kuwa, kwa sasa ndugu yake huyo; "Amerejea baada ya kuruhusiwa".

Ivory Coast inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa huo nchini Afrika Kusini, imepangwa katika Kundi la Kifo la D, linalojumuisha mataifa ya Togo, Algeria na Tunisia.

Katika maandalizi yao ya mwisho kuelekea fainali hizo, Ivory Coast inatarajkia kupimana ubavu na Misri hapo Januari 14, kabla ya kutua nchini Afrika Kusini – ambako itacheza mechi yake ya ufunguzi hapo Januari 22 kwa kuwavaa Togo ‘The Hawks’.

No comments:

Post a Comment

Pages