Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Awadhi ‘Blad Key’ amewataka wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya burudani ambazo amewaandalia.
Licha ya kuwa na vibao vingi, Blad key alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Vimepanda bei’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
Akizungumza Dar es Salaam, Blad Key alisema ananyimbo tatu ambazo tayari amezitengeneza, yupo katika mchakato wa kuzichagua ipi itangulie na ipi ifuate.
“Nimetyengeneza nyimbo tatu mfululizo zenye ujumbe tofauti, sijajua ni ipi itangulie kutoka na bado sijazipatia majina nafikiri wiki ijayo nitakua nishazitafutia majina,” alisema Abdukiba.
Blad Key anaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuzipokea kazi hizo ambazo anasema anauhakika zitafanya vizuri kutokana na ujumbe zilizobeba ndani yake.
No comments:
Post a Comment