JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemzuia Diwa wa Kata ya Kimara Pascal Manota (Chadema), kufanya mkutano wa hadhara kwa madai ya ujio
wa Rais siku ya Jmaa tano.
Akizungumza na Habari Mseto Blog jijini Dar es
Salam leo, Manota alisema huo ni muendelezo wa jeshi hilo kutumika vibaya
zaidi kwa kulinda maslahi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema alimshangaa Mkuu wa Kituo cha Polisi
Kimara, Papalika kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa rais anatarajiwa kutafanya
ziara katika eneo hilo siku ya Jumatano ambapako haieleweki ziara hiyo
inauhusiano gani na mkutano wa jana.
“Sasa huu ni ubabaishaji na hii inadhihirisha
wazi kuwa jeshi hili haliko kwa
kusimamia haki bali lipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya CCM ambapo tunawataka
watuache tupambane wenyewe sisi na CCM katika majukwaa ya kisiasa si kuwasaidia”alisema
Manota.
Hata hivyo, Manota, alisema eneo la Golani
alilokuwa afanyie mkutano liko mbali na kule atakako tembelea Rais, ambako atafanyaa
uzinduzi wa daraja ambalo wananchi wanadai kuwa ni bovu kutokana na kujengwa chini
ya kiwango.
“Huu ni mchezo wa CCM kwani wameona nataka
kuzungumza na wananchi kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo mchakato wa katiba pia
kuelezea matumizi ya fedha za maeneleo ya kata hiyo jinsi zinavyotumika vibaya
ikiwemo na ujenzi wa daraja hilo”alisema Manota
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo,
Charles Kenyela, kutoa ufafanuzi kuhusu mvutano huo, alisema haamini kama kweli
diwani huyo aliandika barua kweli.
Alisema kama angeandika barua hiyo, ni lazima
mkuu wa kituo hicho cha Kimara angefikishiwa kopi kwa ajili ya uthibitisho kuwa
chama hicho kingekuwa na mkutano.
Kenyela alisema hairuhusiwi mtu yeyote
kufanya mkutano bila ya jeshi la polisi kupewa taarifa, ili jeshi hilo liweze
kutoa ulizi kwa ajili ya kuzuia vurugu endapo zingetokea.
Hata hivyo, kama wanadai wamechezewa rafu
yeye ndiye RPC wanayo haki ya kufikisha taarifa hizo kwake ili wa angalie ni
kwa nini imekuwa hivyo na wanaweza kukata rufaa mbele kama hawataridhika na
maamuzi yake.
Ni hivi karibuni jeshi hilo lilizuia maandamano
na mkutano wa Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema), kwa madai kuwa maeneo
waliokuwa wakitaka kupita kuna ujenzi wa barabara hivyo yangeweza kusababisha
foleni na usumbufu kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment