Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday
Mangu ‘Linex’ anatarajia kufanya shoo inayokwenda kwa jina la ‘Usiku wa
Mahakama ya mapenzi’ Jumapili katika ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es
Salaam.
Mahakama ya Mapenzi ni kati ya nyimbo za msanii
huyo ambayo inafanya vizuri katika soko hilo kutokana na mashairi yaliyobeba
ngoma hiyo.
Akizungumza na jijini Dar es
Salaam jana, linex alisema katika shoo hiyo atasindikizwa na wakali wa muziki
huo, H.Baba, Banana Zorro, Kala Jeremiah na wengineo.
Akizungumzia kuhusu uandaaji wa video ya kazi
hiyo, Linex alisema kuna watu ambao ni raia wa Europe ambao anataka
kushirikiana nao katika video hiyo na sasa yupo katika hatua za mwisho za
kukamilisha mazungumzo.
“Unajua msanii unatakiwa kuwa mbunifu, hivyo
nilipenda video ya kazi hii nifanye na watu hao ambapo tukielewana itakua
hivyo, na ikishindikana nifanya na Adamu Juma,” alisema Linex.
Mbali na hayo Linex alisema kwasasa ameamua
kufanya kazi na wasanii wakike ili kuwapa sapoti katika kazi zao na kukuza
muziki huo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment