Na Elizabeth John
BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mkali wa
muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Mohamed ‘Z. Anto’ usiku wa Pasaka
anatarajia kutambulisha kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tanzania’.
Akizungumza Dar es Salaam, Z.Anto alisema
kazi hiyo ataitambulisha katika ukumbi wa Mnyaru nite club uliopo jijini
Arusha.
“Nashukuru mungu kwa kupata shoo hii ambayo
itanipa nafasi ya kuitambulisha ngoma yangu mpya, tukiwa na kundi zima la Solid
Ground Famili kutoka Mabimbo jijini Dar es Salaam,” anasema.
Z.Anto anawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa
wingi siku hiyo ili waweze kupata burudani iliyoenda shule kutoka kwake na
kundi hilo ambalo lililiteka soko la muziki huo kipindi cha nyuma.
Mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha
‘Kisiwa cha Malavidavi’ licha ya kuwa na vibao vingi ambavyo vilivyofanya
vizuri katika soko la muziki huo.
No comments:
Post a Comment