Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Career Company (GCC) ya nchini Uingereza Sarah Roe
(kulia) akipeperusha bendera ya benki ya Exim kwenye kilele cha Mlima
Kilimanjaro maarufu kama ‘Uhuru Peak’ wakati wa upandaji wa mlima huo kwa
hisani ya kuchangia maendeleo ya elimu Barani Afrika. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim Tanzania imedhamini watalii tisa kutoka kampuni yaGlobal Career Company (GCC) ya nchini Uingereza kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni mkakati wa kusaidia kutangaza mlima huo. Upandaji huo wa hisani unalenga kusaidia maendeleo ya Elimu Barani Afrika katika jamii zisizojiweza huku pia ukilenga kutangaza utalii wa Tanzania.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant jijini Dar es Salaam jana ilisema kuwa udhamini huo unalenga kuutangaza utalii wa mlima huo katika nchi za nje.
Grant alisema kuwa sita kati ya watalii hao ambao hawakuwa na uzoefu wa kupanda milima waliweza kufikia kilele cha mlima Kilimanjaro maarufu kama ‘Uhuru Peak’ mapema asubuhi jana na kuipeperusha bendera ya benki ya Exim.
“Tunafuraha kuwa watalii tuliowadhamini wameweza kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Tunaimani kuwa watalii hawa kutoka nje watakuwa mabalozi wazuri katika kuinadi Benki ya Exim na Tanzania kwa ujumla wakirejea nchini kwao,” Grant alisema. Grant alisema kuwa benki yake imejidhatiti kuendelea kutoa misaada mbali mbali ya kusaidia maendeleo ya utalii wa ndani nchini.
Naye Mkrugenzi ya GCC Sarah Roe alisema kuwa “Hi ni fursa ya kipeke kuweza kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro. Masaa 48 ya mwisho yamekuwa na ugumu ila tunashukuru mungu hatimaye tumeweza kutimiza ndoto yetu. “Tunaishukuru Benki ya Exim kwa msaada walioutoa na tutaenda kuwa mabalozi wazuri kwa Benki ya Exim na Tanzania kwa ujumla,” aliongeza
Roe.
No comments:
Post a Comment