HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2013

Mwanakijiji Kalenga awakumbuka wajawazito Hospital teule ya Iringa awapa msaada wa vitanda

Na  Francis Godwin ,Iringa

MKAZI  wa  Kalenga wilaya ya  Iringa  mkoani  hapa Bw Jackson Kiswaga ametoa msaada  wa  vitenda viwili vyenye  thamani  ya Tsh milioni 3.6 kwa  Hospital teule  ya wilaya  ya Iringa Hospital  ya Ipamba ili  kunusuru wanawake  wajawazito kujifungulia chini.

Kiswaga ambae  pia  ni  mkuu wa  M-Pesa  na ukuzaji  wa biashara alikabidhi  msaada  huo  jana mbele ya uongozi  wa Hospital  hiyo na viongozi  wa kata  hiyo ya Kalenga .

Bw  Kiswaga alisema  kuwa amelazimika  kutoa msaada  huo  wa  vitanda  katika Hospital  hiyo  kama njia ya  kuhamasisha  wakazi wengine  wa wilaya ya Iringa ambao wapo nje ya  mkoa  wa Iringa kujenga  utamaduni  wa kuchangia  shughuli  za  kimaendeleo katika wilaya  hiyo  ya Iringa  na mkoa kwa ujumla badala  ya  kuendelea  kuiachia  serikali  na  wahisani  kufanya kila jambo hata yale ambayo  yapo chini  ya  uwezo  wa  wananchi  wenyewe.

"Kuna  baadhi ya  shughuli  za kimaendeleo hazipaswi kusubiri  serikali  wala kusubiri wafadhili  kutoka  nje ya  Tanzania ...tujikipanga wenyewe  wananchi  tunaweza  kufadhili shughuli  hizo   huku  serikali na  wahisani  wakubwa  tukiwasubiri kwa mambo makubwa ambayo  sisi  wananchi hatuwezi  kuyafanya "alisema  Kiswaga 

Kuwa akiwa  kama mkazi  wa jimbo la Kalenga alipata  kulazwa  katika  Hospital  hiyo na moja kati ya  changamoto  kubwa alizokutana  nazo  hapo ni pamoja na suala la upungufu  wa vitanda na changamoto  nyingine  nyingi hivyo kulazimika kwa upande  wake  kwa  kushirikiana na marafiki  zake  waliopo jijini Dar es Salaam  kuchangishana  fedha  za  kununua vitanda  hivyo  vya kisasa  ili  kusaidia  kupunguza uhaba  wa  vitanda .

Aidha  alisema  kuwa ataendelea  kuangalia  uwezekano  wa  kuisaidia  zaidi Hospital  hiyo  ambayo ni mkombozi mkubwa  kwa  wakazi  wa  jimbo la Kalenga na  wilaya ya Iringa  kwa ujumla na  kuahidi  kusaidia  kuingiza maji katika  chumba  cha  kuhifadhia maiti katika  Hospital  hiyo ambayo ina chumba  chenye  uwezo wa  kuhifadhi maiti sita  pekee ila hakuna maji ya  kusaidia  kuosha maiti .

Hata hivyo alisema  kuwa msaada  huo  umelenga kusaidia  jamii ya wana Kalenga na mkoa  wake wa Iringa na  hauna malengo  ya  kisiasa  na  kuwa  baadhi ya  watu   wamekuwa na dhana  potofu  kuwa mtu anapojitolea  kusaidia  shughuli za kimaendeleo nyumbani kwake kuwa anataka nafasi ya  kisiasa na kuwa katika  hili mbunge wa  jimbo  hilo la kalenga Dr Wiliam Mgimwa anatambua msaada  huo .

Kwa  upande  diwani  wa  viti maalum Tarafa  ya  Kalenga Shakra Kiwanga akishukuru  kwa  niaba ya  wakazi  wa Kalenga  alisema  kuwa  msaada  huo ni chachu kwa  wadau  wengine  kuendelea  kufika  katika  Hospital  hiyo na  jimbo la Kalenga  kuendelea  kusaidia  shughuli mbali mbali  za kimaendeleo na kumpongeza Bw Kiswaga  kuwa amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika tafara  ya kalenga .

" Sisi kama  wana  kalenga  tunaendelea  kukuombea  afya  njema na Mungu azidi  kukuongezea  pale  unapopunguza kwani huu ni msaada wa kwanza kutoa kwetu  ulipata  kutusaidia ujenzi wa vyumba viwili  vya madarasa katika shule ya  Sekondari ya Lipuli ....na maeneno mengine  mengi "alisema Bi kiwanga 

No comments:

Post a Comment

Pages