HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 03, 2016

BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA

Ofisa Uhusiano Mwandamizi Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Wilfred Miigo akiwakaribisha wageni waalikwa na waandishi wa habari, waliohudhuria kwenye wa Bodi ya Shirika katika kuelezea mikakati yake ya kiutendaji kwa ajili ya kulikwamua shirika hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.
Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika kuzungumza na waandishi wa habari katika kuelezea mikakati mbalimbali ya kulikwamua shirika. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi, Haruni Kondo na kulia ni Katibu wa Shirika na Bodi, Rochus Assenga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika kuelezea mikakati mbalimbali ya kulikwamua shirika. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga na kulia Katibu wa Shirika na Bodi, Rochus Assenga.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mikakati ya kulikwamua shirika hilo.
Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta na waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa, wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta, Bibi Khadija Shaaban, akinukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dk. Haruni Kondo (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati akielezea mikakati mbalimbali ya kulikwamua shirika hilo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari, wakati alipotakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (wa pili kushoto) kutoa uafafanuzi kuhusu moja ya nyumba ya shirika hilo.
Baadhi ya Wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari. 
Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Posta, Bibi Fatuma Bakari pamoja na baadhi ya Wakuu wa vitengo vya shirika wakifuatilia maelezo yaliyokuwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo, kabla ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Pages