September 27, 2013

PETER MSECHU AWAFARIJI WAKENYA

Na Elizabeth John


KUTOKANA na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea nchini Kenya, Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, amesambaza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kenya Itadumu’ kwa lengo la kuwafariji.




Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msechu alisema kitendo walichofanyiwa wenzetu ni cha kinyama sana, ameguswa na tukio hilo ndio maana ameamua kuwafariji kwa kuwapa burudani.

“Mimi kama msanii ninauwezo wa kufanya lolote ili wapate faraja najua kwa kufanya hivi watafarijika kwa kiasi fulani, kwa asilimia kubwa tunatakiwa kuwapa faraja majirani zetu,” alisema.

Alisema mbali na kazi hiyo, yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao chake kipya ambacho bado hajakipatia jina kutokana na ubora wa kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri ndani na nje ya nchi.


Msechu alishawahi kutamba na vibao vyake kama ‘Kumbe’, ‘Kibudu’ na vinginevyo ambavyo vilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Pages