Na Elizabeth John
KUTOKANA na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea
nchini Kenya, Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, amesambaza
kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kenya Itadumu’ kwa lengo la kuwafariji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msechu
alisema kitendo walichofanyiwa wenzetu ni cha kinyama sana, ameguswa na tukio
hilo ndio maana ameamua kuwafariji kwa kuwapa burudani.
“Mimi kama msanii ninauwezo wa kufanya lolote
ili wapate faraja najua kwa kufanya hivi watafarijika kwa kiasi fulani, kwa
asilimia kubwa tunatakiwa kuwapa faraja majirani zetu,” alisema.
Alisema mbali na kazi hiyo, yupo katika hatua za
mwisho za uandaaji wa kibao chake kipya ambacho bado hajakipatia jina kutokana
na ubora wa kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Msechu alishawahi kutamba na vibao vyake kama ‘Kumbe’,
‘Kibudu’ na vinginevyo ambavyo vilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia
ya muziki huo.
No comments:
Post a Comment