HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 22, 2013

SIMBA, MBEYA CITY ZAINGIZA MIL 123/-

 Kikosi cha Mbeya City.
Kikosi cha Simba.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.

Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

Pages