Ndege iliyobeba mwili wa Marehemu, Sheikh Athuman Magee.
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa akielekea kwenye Ndege kuongoza waombolezaji.
Waombolezaji wakisubiri mwili kushushwa.
Gari la JWTZ likiwa tayari kwa ajili ya kubeba mwili wa Sheikh wa Mkoa wa Mara, Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa Januari 28.
Waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wananchi wa mji wa Musoma wakiwa Uwanja wa Ndege.
Afidh Waziri mmoja wa watu waliotoka na Wmwili wa sheikh Magee Dar akiangaliana rubani wa ndege.
Waombolezaji.
Mwili ukipelekwa nyumbani.
Msafara wa mwili wa Sheikh magee ukielekea nyumbani kwake.
Msagara wa pikipiki ukisindikiza.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, akiwasili nyumbani kwa Sheikh Magee.
Mwili ukishushwa.
Baadhi ya waombolezaji.
MARA, Tanzania
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya
Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara
Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya
Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu
na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya
kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa
nchini India kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege
Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema wamepata pigo kubwa
kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika
kuhimiza masuala ya dini.
Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
PICHA/HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
No comments:
Post a Comment