Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeshauriwa kuboresha huduma mbalimbali katika hospitali zake nchini ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano vinavyotokana ukosefu wa vifaatiba.
SERIKALI imeshauriwa kuboresha huduma mbalimbali katika hospitali zake nchini ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano vinavyotokana ukosefu wa vifaatiba.
Kauli hiyo ilitolewa jijini
Dar es Salaami, Brigedia Mstaafu,
Haroun Othman wakati wa sherehe za kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka
2014, zilizoandaliwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Vijibweni,
Kigamboni jijini.
Alitaja baadhi ya mahitaji
kuwa ni uhaba wa dawa, vifaatiba pamoja na madaktari, wauguzi na hata mazingira
ya wafanyakazi nayo sio mazuri kiutendaji.
“Pamoja na changamoto
mbalimbali zinazochangiwa na mazingira magumu bado hospitali hii yaVijibweni
inatoa huduma nzuri na kwa ufanisi wa hali ya juu jambo linaloifanya ijivunie mafanikio
yake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006,”alisema Othman.
Akizungumza kwa niaba ya
Mganga Mkuu na wafanyakazi, Dk Alfred Mchinamnamba, alisema hospitali hiyo
imekuwa ikiendelea na mpangomkakati wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika
katika hospitali hiyo.
Aliongeza kuwa kwa wale
wanaohitaji matibabu zaidi hupelekwa katika hospitali ya wilaya Temeke ama
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha, Mchinamnamba,
aliwaomba baadhi ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo, wakati mwingine wawe
wavumilivu kutokana na changamoto wanazokumbana nazo kwani nyingine
zinasababishwa na idadi ndogo ya wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment