Rais
Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na
Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi
hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid
Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa
ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26,
1964.
Naye
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed
Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa
Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza
kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public
Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Rais
Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na
Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi
hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid
Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa
ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26,
1964.
Naye
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed
Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa
Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Imetolewa
na;
KURUGENZI YA
MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es Salaam.
12 January, 2014
No comments:
Post a Comment