WALIMU wa Shule ya Msingi ya NDC – NARCO, wanatuhumiwa kutaka kugawana michango na ada za wanafunzi mara zitakapolipwa.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa mtandao huu umebaini kuwepo tuhuma za Mpango huo ulioratibiwa na mmoja wa Walimu aliyekuwa kwenye Kikao cha Walimu Wakuu mkoani Dodoma, ambapo inadaiwa aliporudi aliwashawishi wenzake wakitembelewa na Kiongozi wa Elimu mkoani watoe dai hilo.
Chanzo chetu nje ya kikao kimedai, Mwalimu aliyehudhuria Mkutano akuwa Mwalimu Mkuu, hivyo akiwa Dodoma alipenyeza wazo hilo kwa mmoja wa Viongozi wa mkoani afike shuleni kwao, ili watoe shida hiyo kumkomoa Mwalimu Mkuu ambaye hakuhudhuria kikao hicho.
Wazazi waliohojiwa kwa nyakati tofauti kuhusu hatua hiyo, wamelalamika kwamba wametozwa Mchango wa Sh. Laki 100,000/- kila mwanafunzi walioulipia kupitia NMB Akaunti Na. 503100014161- NARCO-Tumaini Hostel kwa ajili ya Ujenzi, ili hali wakijua ugumu wa maisha.
Wamedai, wanashangaa kuchangishwa fedha hizo kwa sababu Mkuu wa Mkoa Dk. Rehema Nchimbi, aliita wadau wakaichangia Shule hiyo na wengi wao wanadai walishiriki kuchangia wakiwemo Wabunge ambao awali walitangulia kuchanga kabla ya Nchimbi na wadau.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya NARCO, Sperancia Mnyanyika, alipotafutwa mara kadhaa katika Simu yake 0764094366 kabla hatujaenda mitamboni, ili afafanue juu ya Sakata hilo hakupatikana, lakinini chanzo chetu cha pili kilisema ana matatizo ya kifamilia kijijini kwao.
Katika uandikishaji wa darasa la kwanza, wazazi mkoani Morogoro walipigana na kulaani kulipishwa michango Sh. 50,000/-, Ingawa akiwa bungeni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Kasimu Majaliwa, aliwaonya Walimu Wakuu kuhusu Michango akisema atakayevunja Sheria ataadhibiwa.
No comments:
Post a Comment