February 17, 2014

Mahabusu Tunduma ajinyonga
Na Kenneth Ngelesi, Mbeya

WATU wawili wamefariki dunia likwemo tukio mahabusu kujinyonga  kwa kutumia tambala la kuedekia katika kituo cha polisi cha Tunduma Wilayani Momba Mkoani Mbeya.

Tukio la kwanza limetokea Februali 17 mwaka huu majira ya saa 06:00 asubuhi ambapo mahabusu aliyefahamika kwa jina la Vumi Elias (30) mkazi wa mtaa wa maporomoko Tunduma wilaya ya Momba,

Taarifa zinaeleza kuwa marehemu alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa kituo cha afya tunduma baada ya kujaribu kujinyonga akiwa ndani ya mahabusu katika kituo cha polisi Tunduma.

Kwa mujibu wa taarifa la jeshi la Polisi zinaeleza kuwa  marehemu aliingia katika choo cha mahabusu kilichopo ndani ya mahabusu hiyo majira ya saa 04:30 usiku na kutaka kujinyonga kwa kutumia tambala la kupigia deki.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa  marehemu aliokolewa na askari waliokuwa zamu chumba za mashitaka na kukimbizwa kituo cha afya kwa matibabu akiwa katika hali mbaya na hawezi hata kuongea baada ya kupata taarifa kutoka kwa mahabusu wengine walioingia chooni humo.

Marehemu  huyo alifikishwa hapoa  mnamo Februali 14 mwaka huku akiwa amekamatwa  kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa Polisi ACP Robert Mayala chanzo kinachunguzwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika kituo hicho cha afya.

Aidha katika tukio la pili mama mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Maria Mwawangu (56) mkazi wa kijiji cha Upendo alikutwa ndani ya nyumba yake ameuawa kwa kunyongwa shingo baada ya kubakwa na watu wasiofahamika.

Tukio la hilo lilitokea mnamo Februali 16 mwka huu  majira ya usiku na mwili wa marehemu ulikutwa majira ya saa 13:30 mchana huko katika kijiji cha Upendo wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya.

Taarifa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa anaishi peke yake katika nyumba hiyo na chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa.

Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi wa polisi Robert Mayala anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mtu waliohusika na tukio hili azitoe kwa jeshi la polisi ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

No comments:

Post a Comment

Pages