NA KENNETH
NGELESI, MBARALI
MICHUANO ya
soka ya Merere cup 2014 ilifikia tamati jana huku timu ya soka ya Kapunga FC
kutoka kata Itambo ikiibuka bingwa na kuondoka na kombe baada ya kuichapa timu
ya Soka Motor Cycle kutoka kata ya Chimala kwa jumla ya mabao 2-1 katika
pambano la fainali lililo pigwa juzi katika uwanja wa Chimala.
Mchezo huo
ambao ulikuwa mkali huku wachezaji wa timu zote mbili wakionyesha utundu wa
kusakata soka, Kapunga ndiyo walio kuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani
wao kupitia kwa mchezaji Shavi Maketa kwani dk 6 ya mchezo aliindikia timu yake
bao la kwanza.
Baada ya ya
Kapunga kupata bao hilo liliamsha hasira kwa wachezaji wa timu ya Waendesha
bodaboda (Moter Cycle)na kuanza kulisakama lango la wapinzani dakika 10
walipata bao la kufutia machozi kupitia kwwa mchezaji Philipo Philipo kwa njia
ya mkwaju wa penanti ambayo ilipatikana baada ya beki wa timu ya Kapunga
kumungusha katika eneo la hatari na hadi mapumziko mabao yalikuwa 1-1.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikisaka goli la kuongoza hata hivyo Kapunga
FC ndiyo walikuwa makini kuzitumia nafasi kwani dk 75 ya mchezo waliandika bao
la pili na la ushindi ambalo liliewekwa kimyani na mchezaji Bahati Msofya na
hadi dk 90 zinamalizika na mwamuzi Devid Malema alipuliza filimbi ya mwisho
Kapunga Fc 2 na Motor Cylce 1.
Katika
fainali hizo timu ya Kapunga aliwatoa Rajabu Alex,Meja Manyanya, Geofrey
Philimon,na Frorence Chitoto huku nafasi zao zikichukuliwa nma Mbaraka
Muba,Maiko Michael,Exaurd Edward na Simon Mwampamba.
Wakati huo
huo timu ya Motor Cycle waliwatoa Minjiro Alimwene,Rajabu Ngaile na Damas Elius
huku nafasi zao zikichukuliwa na Joseph Ngondwa Baraka Cheusi,na Mbaraka Muba.
Mara baada
ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulifanyika katikia Uwanja wa Chimala Mgeni
mgeni rasmi katika fasdinali hizo zilizo andaliwa na shirika nla hifadhi za
taifa (TANAPA) Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi aliwa kabidhi washindi
zawadi.
Zawadi hizo
katika fainali hiyo bingwa alifanikiwa kuondoka na Kombe,Fedha,shilingi lakini
tano,seti mopja ya jezi,ma mpira mmoja Ungo wa televisheni ulio tolewa na
kampunio ya Azamu TV.
Mbali na
zawadi hizo kwa mshindi wa kwanza lakini pia waandaaji wa mashindano hao
walitoa zawadi kwa mshindi wa pili ambao ni Motor Cycle seti moja ya
jezi,shilindi laki 300,000/ na mpira mmoja wakati msindi wa tatu alizawadiwa
shilingi laki mbili.
Akizunngumza
mara baada ya kukabidhi zawadi Kocha Mwambusi aliwapongeza waa ndaji wa michuano hiyo yenye lengo kumkumbuka
chief Merere pamoja kupiga vipa Ujangiri kwani imesadia kuibua vipaji.
Mbali na hilo
lakini pia aliwataka wachezaji kuendelea kujituma katika michuano mbalimbali inayo
andaliwa na wadau wa mchezo huo kwani ndiyo njia pekee ya kuabaini vipaji vyao
ambapo wakifanya vizuri itakuwa fursa kwao kupata timu za ligi kuu.
Kwa upande
wake mratibu wa michuano hiyo William Ndondole alisema kuwa lengo la kufanyika
kwa m ichuano hiyo ni kuwafanya vijana wasijiingize katika masuala mouvu na
kwamba michuano hiyo ilidhamiwa na Benki ya Posta,Azam TV,Tanapa,kupitia
hifadhi ya Taifa ya Ruhaha.
No comments:
Post a Comment