October 10, 2014

KINANA MUFINDI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika leo, Oktoba 9, 2014 kwenye  Uwanja wa Mashujaa, mjini  Mufindi akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama mkoani Iringa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Vijana wa CCM alipowasili wilayani Mufindi mkoani Iringa
 Kinana akisalimiana na Mbunge wa Mufindi Kusini Menradi Kigola wakati wa mapokezi hayo. Kulia Katibu wa CCM wilaya Mufindi Mtaturu.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiangalia namna mbao zinavyotayarishwa kwenye kiwanda cha mbao cha Emmanuel Investiment, kinachomilikiwa na Ndugu Charl Ayo, mjini Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa
 Katibu Mkuu wa CCM akikagua kiwanda hicho cha upasuaji mbao
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama mti uliopandwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye Ofisi za Kampuni ya Sao Hill, wilayani Mufindi alipotembelea kampuni hiyo. Mto huo ulipandwa na Mwalimu Nyerere zaidi ya miaka 30 iliyopita.
 Mti wa Mwalimu Nyerere ulivyostawi Sao Hill
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Kampuni ya Sao Hill
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Ofisi za Kampuni ya Sao Hill, Mufindi
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sao Hill wakimpokea Kinana alipotembelea kampuni hiyo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo kwenye mkutano mkuu wa CCM jimbo la Mafinga Kaskazini.
Baadhi Wajumbe waliohudhuria mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mafinga Kaskazini
 Viongozi wa Dini wakiwa kwenye mkutano mkuu wa CCM jimbo la Mufindi Kaskazini
 Mwenyekiti wa Wazee Waasisi wa CCM wilaya ya Mufindi Mzee Raphael Ngogo akisoma risala ya Wazee kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Wajumbe wakiimba nyimbo za kumkaribisha Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa Dini wilaya ya Mufindi ambao walialikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Mufindi Kaskazini.
 Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mufindi Dk.Boaz Mnenegwa  akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea wodi ya kina mama hospitalini hapo.
 Sehemu ya Wodi ya akina mama katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.

No comments:

Post a Comment

Pages