HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2014

LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA, MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA CITY 2-0

Mshambuliaji wa timu soka ya Mtibwa sugar Mussa Mgosi akidhitiwa na Mabeki ya Mbeya City,Kenny Ally kushoto na Deogratius Julius kulia katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jana katika uwanja wa Sokoine jiji Mbeya (Picha na Kenneth Ngelesi)
 Beki wa timu ya Mbeya City, Deogaritus Julius akiambaa akimiliki mpira huku akinyelewa na mshambuliajai wa Mtibwa Sugar, Mussa Mgosi katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Kumbu kumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji wa timu ya Soka ya Mtib wa wakishanglia goli lao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ulipigwa na katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
TIMU ya Mtibwa Sugar, leo imeendeleza wimbi la ushindi na kubaki kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu, baada ya kuifunga Mbeya City ya Hapa kwa mabao 2-0 katika pambano kali kwenye Uwanja wa Sokoine.

Ushindi wa leo umeiweka juu zaidi timu ya Mtibwa Sugar kwa toafuti ya pointi tatu, baada ya kuifanya kufikisha pointi 13, huku ikiziacha Yanga na Azam FC zikibanana katika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 10 baada ya mechi tano tano kwa kila kikosi tangu kuanza kwa msimu huu wa 2014/15.

Bao la kwanza la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 20 na nyota wake Ame Ally, akiunganisha kona iliyopigwa na beki wa kushoto wa zamani wa Yanga anayekipiga na ‘Wakata Miwa’ hao kwa sasa, David Luhende. Baada ya bao, Mtibwa waliendelea kuishambulia Mbeya City na nusura wapate bao la pili dakika ya 31 kupitia Ally Shariff. hadi mapumziko, matokeo yalikuwa wageni kuongoza mechi kwa bao hilo 1-0 dhidi ya wenyeji wao ambao msimu huu unaonekana kuwa mgumu kwao.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake Mbeya City wakipania kusawazisha bao, ambako walianza na badiliko la kumtoa Themi Felix na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Malyanzi, ambaye nusura aipatie timu yake bao la kusawazisha, lakini shuti lake dakika ya 53 lilidakwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.

Dakika ya 76, Mtibwa wakajihakikishia ushindi muhimu, kutokana na bao maridadi la Andrew Vicent, alilofunga baada ya kuwalaamba chenga mabeki wa Mbeya City na kufumua shuti kali na kumshinda kipa David Burhani.

Dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Hashimu Abdallah wa Dar es Salaam, Mtibwa nusura wapate bao la tatu, lakini shuti la adhabu ndogo nje ya boksi, iliyotokana na Vicent kuchezewa rafu, kupaa nje ya lango. Hadi mwisho, Mtibwa Sugar 2 Mbeya City 0.


Vikosi katika pambano hilo vilipangwa hivi, Mbeya City: David Burhani, Kenny Ally, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yohana Morris, Yusuph Abdallah, Deus Kaseke, Steven Mazanda, Paul Nonga, Saad Kipanga na Themi Felix.

Mtibwa Sugar: Mtibwa Sugar, Said Mohammed, David Luhende, Salim Mbonde, Andrew Vicent, Shabani Nditi, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Mohammed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na Ally Shariff.

No comments:

Post a Comment

Pages