Na Mwandishi Wetu
OFISI ya
Taifa ya Takwimu (NBS),imesema mfumuko wa bei
katika kipindi cha Septemba mwaka huu umepungua kutoka asilimia 6.7 hadi
6.6 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi Agosti.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za
uchumi na Jamii, Ephraim Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka kutoka
sh. 140.61 katika kipindi cha wa Septemba mwaka jana hadi sh 149.9, Septemba mwaka huu.
Alisema hali
hiyo imechangiwa na kupugua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa
zisizo za vyakula kwa kipindi cha Septemba mwaka huu na Septemba ya mwaka jana.
“Hii
inaamanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioishia Septemba mwaka huu imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa
mwaka uliyoishi kipindi cha Agosti mwaka huu.
“Mfumuko wa
bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi nao umepungua hadi asilimia 8.5
mwezi Septemba mwaka huu kutoka asilimia 8.8 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi
Agosti mwaka huu,”alisema Kwesigabo.
Kwesigabo,
alisema mfano, mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua
katika kipindi cha Septemba 2014 zikilinganishwa na bei za Septemba mwaka jana
kuwa ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 7.7, mahindi (asilimia 8.3), ulezi
(asilimia 5.5), matunda (asilimia 5.0), na sukari.
Kwa upande
mwingine, bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua bei katika kipindi cha Septemba
mwaka huu zikilinganishwa na bei za Septemba mwaka jana ni pamoja na sare za
shule kwa asilimia 4.9, simu za mkononi (asilimia 1.7, runinga (asilimia 2.8),
na viatu (asilimia 1.2).
“Mfumuko wa
bei wa Septemba mwaka huu unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa
asilimia 0.4 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.0 mwezi Agosti,” alisema
Kwesigabo.
Aidha, uwezo
wa sh 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh 66.70 katika
kipindi cha Septemba mwaka huu kutoka Septemba mwaka 2010.
Akizungumzia
mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kwesigabo alisema,
unamwelekeo unaofanana na nchi nyingine.
Alisema
mfano; mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi asilimia 6.6 katika kipindi
cha Septemba kutoka asilimia 8.36,
Agosti mwaka huu na nchini Uganda uliendelea
kupungua hadi asilimia 1.4 kutoka asimia 2.8 katika kipindi hicho hicho.
No comments:
Post a Comment