Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Madaktari Bingwa wa Macho nchini kimewataka Watanzania
kujenga tabia ya kuchunguza afya ya macho ili kuepuka upofu usio walazima.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama hicho, Dk. Neema Kanyalu, wakati alipokuwa
akizungumzia Siku ya Macho duniani, ambapo leo ndio kilele chake.
Alisema, kuna baadhi ya matatizo ya macho yanatibika kirahisi endapo
mgonjwa atafika hosipital mapema na kfanyiwa ucgunguzi wa afya jicho.
“Macho ni kiungo
muhimu katika mwili kama vilivyo vingine kwa binadamu, ambapo yakipata matatizo
ni vema mgonjwa akamwone daktari kwa ajili ya kupata tiba, na hata kwa wagonjwa
wa kisukari, nao wanapaswa kuwaona watalaamu kwa ajili ya matatizo hayo ambayo
husababisha macho kupata upofu.
“Matatizo ya macho yanatabi kinachohitajika ni kwa
wagonjwa kujitahidi kufika katika hospitali mapema hali itakayowaidia kuwaepusha
kupata upofu,”alisema Dk. Neema.
Dk Neema, alivitaja Vituo ambavyo vitahusika katika
kutoa huduma ya uchunguzi wa macho na maradhi ya kisukari kuwa nikatika
hospitali ya Ilala, Temeke na Mwananyamalautoaji.
Aidha, alitoa rai kwa wagonjwa wenye matatizo ya
macho kuwa wanahakikisha wanapata matibabu kutoka kwa madaktari maalumu ambao
walihusika na uchunguzi matatizo yao.
Dk Neema, alisema watakapofanya hivyo, itawasaidia
katika kuwaepusha na matumizi ya dawa zisizo sahihi, hivyo kuwasababishia upofu
baadala ya kuwaponya.
Vilevile, amewashauri baadhi ya akina dada nchini
wanaopenda urembo kuwa makini na vitendo vyao uwekaji vioo bandia katika macho
ili yabadilike rangi na kuwa kama ya wazungu kuwa ni hatari, kutawasababishia
kupata upofu.
Itakumbukwa
kwamba, takwimu za WHO zilizotolewa hivi karibuni zinaonyesha asilimia 80 ya
wagonjwa milioni 45 wa macho wana umri zaidi ya miaka 50 na asilimia 90 ya
wagonjwa hao wanaishi katika nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini ikiwemo
Tanzania.
No comments:
Post a Comment