HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 08, 2014

RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UJENZI YA NSSF

Rais Jakaya Kikwete akimsaikiliza Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli wakati alipotembelea daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Miradi ya NSSF, Mhandisi John Msemo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK. Ramadhani Dau, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka. Daraja hilo linajengwa na NSSF kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha ya Pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Rais Kikete akiwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli wakielekea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mataka akitoa maelezo kwa Rais Kikwete.
Rais Kikwete akiangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Rais Kikwete akikagua daraja la Kigamboni.
Rais Kikwete akikagua daraja la Kigamboni.
Moja yua nguzoi za daraja hilo.
Nguzo za daraja la Kigamboni.
Rais Kikwete na msafara wake wakipita katika daraja la Kigamboni wakati walipofanya ziara ya kukagua miradi ya NSSF.
Nyumba za Mtoni Kijichi.
Nyumba za Mtoni Kijichi.



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Siphia Mjema akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu .
 Rais Kikwete akiwasilia katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 1120 za NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
 Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Miradi ya NSSF, Mhandisi John Msemo.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba 1120 za NSSF zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau. 
  Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba 1120 za NSSF zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
 Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba 1120 za NSSF zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akiangali nyumba za Mtoni Kijichi.
Rais Kikwete akitoa kukagua nyumba hizo.

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza changamoto zilizoainishwa katika ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam, zitatuliwe haraka kabla ya mradi huo kukamilika.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya ujenzi huo, alipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi, alisema kuwa utekelezaji wa mradi unapaswa kwenda sambamba na utatuzi wa changamoto hizo.

Wakati akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa Mradi huo, John Msemo, alisema zipo changamoto chache ambazo zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano na serikali.

Msemo alizitaja changamoto hizo kuwa, ni pamoja na wembamba wa baadhi ya barabara jijini sambamba na msongamano wa magari.
Alitoa mfano wa barabara hizo, ambazo ni Vijibweni-Mjimwema, Bendera Tatu-Kamata na Gerezani- Ohio kuwa ni nyembamba ambazo zinasababisha msongamano wa magari.

Aliongezea kuwa, msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Kilwa - Mandela, Chang'ombe-Mandela na Nyerere (Tazara) kuwa unapaswa kushughulikiwa.

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema tayari serikali imeanza kushughulikia changamoto hizo, ambapo imeongea na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na kutenga fedha katika bajeti ya 2014/15 kwa ajili ya upanuzi wa barabara hizo.

Dk. Magufuli alisema, katika bajeti ya hiyo fedha zimetengwa kulipa fidia kwa ajili ya barabara ya Vijibweni-Mjimwema ili iongezwe upana na kwamba, ile ya Ohio-Gerezani mazungumzo yanaendelea na ADB.

Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ushirikiano wa serikali na wadau na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambalo linatarajiwa kukamilika Juni mwakani, na kuzinduliwa na Rais Kikwete.

Baada ya kutembelea mradi huo, Rais Kikwete alikagua ujenzi wa nyumba 1120 zilizojengwa na NSSF katika eneo la Mtoni Kijichi, ambapo aliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo wa nyumba za watu wa kipato cha kati na chini.

Rais alizindua mradi nyumba hizo na kuiagiza Manispaa ya Temeke kuangalia uwezekano wa kuijenga barabara ambayo itasaidia watumiaji wa nyumba hizo pamoja na kutengeneza miundombinu nyingine muhimu ikiwemo maji na huduma za Afya.

Wakati wa ziara hiyo, Rais ambaye alisherehekea siku yake ya kualiwa jana, alikabidhiwa kadi maalumu ya kumtakia maisha marefu na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau.

No comments:

Post a Comment

Pages