HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2014

Bwawa la Mtera hatarini kutoweka

 Wakazi wa Migoli Mtera  wakiingia na punda katika bwawa la Mtera  ya matumizi nyumbani  baada ya  kina chake  kupungua  zaidi. (Picha na Francis Godwin Blog)
 Wavuvi  wa samaki katika bwawa na Mtera  Iringa  wakichagua samaki  baada ya  kutoka kuwavua katika bwawa  hilo kwa maelezo yao  hali ya upatikanaji wa samaki  imeendelea  kupungua  zaidi na samaki  wakubwa  hawapatikani kirahisi ,pichangine ni mitumbwi iliyoachwa na  wavuvi baada ya kina cha maji  kupungua na baadhi ya maeneo ya  bwawa  hilo kubaki mfano wa mto (picha zote na Francis Godwin Blog)

Na  MatukiodaimaBlogu
KINA  cha maji katika  Bwana  ambalo ni  moja kati ya  vyanzo vya  uzalishaji wa umeme  nchini  lina hali mbaya  baada ya maji  kukauka   na  sasa  kilomita  10  zaidi zageuka  ukame.

Uchunguzi  uliofanywa na mtandao wa matukiodaima.co.tz   umebaini  kuwepo kwa kasi kubwa ya bwawa  hilo  kuendelea kupoteza sifa ya  kuendelea  kuitwa  bwawa  baada ya maji  kuendelea kukauka na  kulifanya sasa  bwawa  hilo kuwa na hadhi ya mto.

Mmoja kati ya  wavuvi  katika  bwawa  hilo Frank Mvili  alisema  kuwa   kupungua kwa  kina cha maji katika  bwawa  hilo  kumechangiwa  zaidi na uharibifu wa mazingira na baadhi ya  watu kulima kwa kutumia jembe la  kukokotwa na ng'ombe pia  uchungaji wa  mifugo katika kingo  za  bwawa  hilo na hatua ya Tanesco kuendelea  kulifungulia bwawa  hilo ni  sababu ya msingi
Kwani  alisema  kuwa  maji   katika bwawa  hilo kwa  miaka mitano  iliyopita  yalikuwa jirani na makazi ya  watu  ila kwa  sasa  maji hayo  yamejivuta  kutoka  eneo la awali umbali wa kilomita 10 na  kufanya  baadhi ya maeneo  kupoteza  sifa ya  bwawa na kuwa mfano  wa mto.

Alisema mbali ya mabadiliko  ya tabia nchi kuathiri  ila bado  serikali imeshindwa  kabisa  kuchukua hatua ya  kulinusuru  bwawa  hilo na uharibifu  unaoendelea kujitokeza.

Kuhusu  shughuli za  uvuvi ambazo zilikuwa  zikitegemewa  zaidi katika  bwawa  hilo Mvili alisema kwa sasa  shughuli  hizo  zimeanza  kupoteza sifa yake  baada ya  samaki kuanza  kuwa adimu  zaidi kupatikana na  waliopo ni  wale wadogo  wadogo na kuwa baadhi ya  wavuvi  wameanza  kufungasha vilango kwenda maeneo mengine ya nje ya mkoa wa Iringa  kwenda  kuendelea na shughuli za uvuvi.

Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba akielezea  kuhusu  bwawa  hilo alisema  kuwa mbali ya  sababu  nyingine  ila  hali ya  mvua  imechangia  maji kutojaa zaidi katika bwawa  hilo na kuwa  suala la uharibifu wa mazingira  umeendelea  kuliathiri  bwawa  hilo.
Hivyo  alisema amepanga  kufanya  ziara  katika maeneo ya  bwawa  hilo  ili  kupata uhalisia  wa bwawa  hilo kwa  sasa na kuweka mikakati mipya ya  kulinusuru.

No comments:

Post a Comment

Pages