Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha
Waaandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepokea kwa masikitiko
taarifa za vifo vya waandishi wawili wa habari za michezo na burudani nchini, Inocent
Munyuku na Baraka Karashani (pichani).
Kwa mujibu wa
taarifa ya Taswa kwa vyombo vya habari ya jana mchana, Baraka alifariki dunia
jana mchana katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa
matibabu.
Baraka amewahi
kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo New Habari (2006) Ltd na
Nipashe.
Taarifa hiyo
iliongeza kuwa, kifo kingine ni cha Munyuku aliyefariki dunia usiku wa kuamkia, leo.
Munyuku
aliyefikwa na kifo akiwa mfanyakazi wa New Habari Ltd, amewahi kufanya kazi
vyombo kadhaa ikiwemo Mwananchi Communications Ltd na Uhuru Publication Ltd.
Kupitia taarifa
hiyo iliyosaniwa na Kamtibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, vifo hivyo ni pigo kwa
waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla.
“Baraka na
Munyuku wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana,” ilisema taarifa
hiyo.
Mhando alisema,
taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za
marehemu mahali pema peponi. Amina.
RIP wadogo zangu
ReplyDelete