NA MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU ya Coastal Union ya Vijana U-20 imepania kuhakikisha
inatetea taji lake
wanalolishikilia la
Michuano ya Kombe la Uhai kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ambayo
yanatarajiwa kuanza hivi karibuni hapa nchini.
Coastal Union U-20 ambao ni mabingwa wa kombe hilo mara baada ya kuifunga Yanga kwenye mechi ya Fainali
ya Mashindano hayo msimu uliopita kwenye mchezo fainali ambao ulichezwa uwanja
wa Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo,Meneja wa timu hiyo,Abdul Ubinde alisema
kuwa maandalizi ya timu hiyo kuelekea michuano hiyo yanaendelea vizuri ambapo
timu hiyo inaendelea na mazoezi yake kila siku kwenye uwanja wa soka Disuza
asubuhi na jioni chini ya Kocha wake,Joseph Lazaro ambaye amepania kutetea taji
hilo.
Ubinde amesema kuwa kwenye mashindano hayo msimu huu timu
hiyo itaingia ikiwa na lengo moja la kuhakikisha wanapambana kufa na kupona ili
kuweza kuendeleza kushikilia ubingwa wake kwa sababu ya uimara wa kikosi hicho.
Amesema kuwa hatuendi
kushindana kwenye michuano hiyo bali kuhakikisha tunatetea taji letu la Ubingwa
wa Michuano hiyo ambao sisi tunaingia kama
mabingwa watetezi.
Ameongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kimeimarika vilivyo na
kipo tayari kushiriki mashindano hayo kwa mafanikio kutokana na kuwa na
wachezaji mahiri wenye uwezo wa kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji nguli akiwemo mlinda
mlango namba mbili wa kikosi cha Coastal
Union inayoshiriki ligi kuu Fikirini Suleiman “Mapara”Mohamed Twaha
“Dijong”,Mtenje Albano na Mohamed Omari “Hungry”
Meneja huyo amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo kwenye
morali wa kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kucheza kwa umakini mkubwa lengo
likiwa kupata matokeo mazuri kila mechi watakayocheza.
No comments:
Post a Comment