HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 02, 2014

VIJANA WAASWA KUJIUNGA NA SKAUTI

NA KENNETH NGELESI, MBEYA 
 
MKURUGENZI wa kampuni ya Tugeme Interprises ya mjini Tukuyu mjini Rungwe,Tumaini Mwaijande amwapongeza wazazi nchini kwa uamuzi wa kuwaruhusu watoto wao kujiunga na skauti licha ya kuwa wanafunzi.

Mbali na wazazi lakini pia alisifia wanafunzi ambao wameamua kujiunga na skauti kwani vijana hao wamekuwa msaada katika shughuli mbalimbali za kijamii hasa katika amasuala ya ulinzi hasa katika palipo na msongamano wa watu.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi huyo katika maafari ya nne katrika Sekondari ya Hoolyweood iliypo katika Mji wa Mlowo Wilaya Mbozi,baada kufanyiwa mapokeza mazuru na kushudiwa shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na vijana hao ikiwemo michezo,uchanjani wa kuni,na kuhakikisha usalamu wakati wote wa maafari hayo.

‘Ndugu zangu kutoka Moyoni nimefurahi sana kuoan shule yenu inaskauti kwani ni imani ytangu vijna hao wanandidhamu ya hali juu na tumeona maala pengine vijna hao ni msaada mkubwa mkubwa katika masualaya ya ulinzi n hata uokoani hivyo niwaombea wale amabo badop hawajiaunga wafanya kila linalo wezekana wajiunge’ alisema Tugeme.

Alisema sababu ya kuwapongeza wazazi hao kwani wangeweza kuwa kawakataza vijna wao kujiunda kwa madai kuwa wamelipa ada kwa ajili ya kusoma na siyo skauti lakini kwa kutambua umuhimu wameruhusi hivyo anamini wametambua sababu moja wapo ya kumfanya mwanafunzi kufanaya vizuri ni nanidhamu na ukakamavu.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo alitoa msaada wa mipira miwili kwa kwa ajili ya netboli na mpira wa miguu, na mifuko kumi ya Saruji kwa kwa ajili ya kisakafia ukumbi wa mikutano wa shule.

Akitoa salamu kwa wazazi wawa wanafunzi wa Shule hiyo Mkurugenzi wa Shule hiyo Izyazi Kameka alisema kuwa ni jambo la kujivunia kwani shule hiyo ilianza ikiwa na wanafunzi sabini tu, lakini kutokana na maendeleo mazuri kitaaluma kumekuwa na ongezeko kubwa na wanafunzi kwa kidato cha kwanza na wale wanao hamia.

Alisema kuwa  katika kipindi cha miaka mitano shule hiyo ina wanafunzi 735 huku wahitimu wa kidato cha nne ambao walianza 54 mwaka 2011 na kufikia wanafunzi 201 ambapo ongezeko hilo ni kutokna na wanmafunmzi walihamia.

Aidha katika risala yao wanafunzi hao ambayo ilisomwa na Baraka Kabenga, walisema kuwa licha ya mafanikio makubwa ya shule hiyo lakini imekuwa ikikabilkiwa na changamoto kadhaa,utoro baadhi ya wanafunzi,ukosefu wa ukumbi wa Mikutano na Zahati kwa ajili ya matibabu hali ambayo inachangia kuadhiri maendeleo kitaaluma.

No comments:

Post a Comment

Pages