Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid akiongea na Wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke, Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo, ambayo lengo lake ni kuwakomboa vijana wa Mtaani pamoja na vipindi vingine vya kuelimisha Jamii na Burudani, Pia amewashukuru kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitasaidia katika Hospitali hiyo leo Tarehe 1.11.2014
Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm iliyo fanyika katika katika Hosipitali Teule ya Mkoa wa Temeke Ambapo Ghetto Radio Imeweza kufunguliwa Rasmi Katika Mkoa huo nakuweza kutoa Msaada Vifaa Mbalimbali pamoja na Madawa Ambavyo Vyote kwa ujumla vimegharimu kiasi Cha Shilingi Milioni sita na Laki sita.
Mkurugenzi wa Ghetto Radio Matt Brouwer akizungumza neno wakati wa uzinduzi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Ambapo Bw.Brouwer Alisema kuwa Ghetto Radio ilianzishwa nchini Kenya Miaka Sita iliyopita nakuweza kuwasaidia vijana mbalimbali Hivyo wameweza kuingia Nchini Tanzania Ilikuendeleza kuwapa vijana Fursa Na elimu INayo Tolewa na Kituo Hicho Kwa Hapa Nchini
Mganga Mkuu wa Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke Amaani K. Malima akitoa neno la Shukurani kwa Timu nzima ya Ghetto Radio ya Sibuka Fm kwa kufanya uzinduzi wa Radio yao katika Hospitali hiyo pia kutoa Msaada wa vitu mbalimbali vitakavyo saidia katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi akiwashukuru Ghetto Radio ya Sibuka FM kwa kuanzisha Kituo hicho pia na wao wametoa vifaa vya matibabu kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo wa Radio
Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Dar es salaam Leonard Masonu akitoa neno la Shukurani
Hivi ni Baadhi ya vitu ambavyo vimetolewa na Ghetto Radio ya Sibuka Fm katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke wakati wa uzinduzi Rasmi wa Radio hiyo
Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid akikabidhiwa Rasmi msaada wa Vifaa na Vitu mbalimbali vitakavyo tumika katika Hospitali teule ya Mkoa wa Temeke kutoka kwa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Waziri wa Afya Mh. Seif Rashid kushoto Akishukuru kwa vifaa hivyo.
Baadhi ya Wadau mbalimbali walioshiriki katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Baadhi ya Wauguzi wakiwa katika uzinduzi huo Rasmi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm pamoja na wadau mbalimbali wakijiandaa kuelekea kutoa Msaada wa vitu mbalimbali katika vyumba vya wagonjwa
Wakiwa wanaelekea Wodini
Kulia ni Mkurugenzi wa Sibuka George Ndagali akiwa katika Wodi ya watoto kukabidhi zawadi za watoto na mama zao, katikati ni Mwanamuziki Mkongwe wa Bongo Flava Juma Nature ambaye ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm Juma Nature akiwa anatandika Shuka moja wapo katika Wodi ya watoto kuashiria kukabidhi mashuka hayo.
Baadhi ya Timu ya wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka Fm
No comments:
Post a Comment