Vijana waliotembea kwa miguu kwa siku 37 kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu vitendo vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya rasilimari za taifa. Vijana hao wamejitambulisha kwa majina ya Juma
Maganga, Halid Suleiman na Atanas Michael,
wakazi wa Nyamagana Wilaya Geita mkoani Mwanza.
Vijana hao wakionyesha mshikamano.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio la kukamatwa kwa vijana hao.
Polisi wakiwa wamewadhibiti vijana hao.
Polisi wakiwazuia waandishi wa habari kusogelea eneo la Kituo cha Polisi Magomeni baada ya kuwatia nguvuni vijana walioandamana kutoka kwa Mwanza kwa miguu hadi Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, linawashikiria vijana watatu waliofanya maandamano bila kibali kwa lengo la kupeleka ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Vijana hao wamefahamika kwa majina ya Juma
Maganga, Halid Suleiman na Atanas Maico,
wakazi wa Nyamagana Wilaya Geita mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya vijana hao kuwekwa choini ya ulinzi wa Polisi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Jordan Rugimbana alisema vijana hao walianza kufanya maandamano Novemba 24 mwaka jana ambapo walianzia Geita na kufika Dar es Salaam leo majira ya asuhuhi.
Vijana haoi huku wakiwa wamevalia nguo zilizoshonwa kwa magunia na kutumia kitambaa cha bendela ya taifa.
Rugimbana alisema lengo la
vijana kufanya maandamano ni kumfikisha ujumbe Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete wa kulaani utumiaji mbaya wa
rasilimali za nchi bila kuwanufaisha wananchi wenyewe.
Lengo lingine ni kulaani
vitendo vya rushwa na ufisadi unaoendelea bila wahusika kuchukuliwa
hatua, kulaani uvunjifu wa haki za binadamu unaoendelea.
Aidha ujumbe wao mwingine ni
kuitaka Serikali ya Tanganyika irudishwe sambamba na kusambaza uzalendo wa
watanzania waweze kupendana na kuwa wazalendo kwa nchi yao.
“Kama kweli wametembea kwa
siku hizo 37 wamevunja sheria kwa sababu hawakuwa na kibali, matembezi hayo
yalikuwa na nia ya kitu fulani hivyo
walipaswa kuomba kibali” alisema Rugimbana
Rugimbana alizuia vijana hao
wasifike Ikulu mpaka wafuate sheria na taratibu.
Baada ya vijana hao kutoka
katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni yaliongoza moja kwa moja na kusema
lazima ujumbe wao ufike kwa Rais Kikwete.
Hali hiyo iliwafanya Polisi
kutumia nguvu na kuwapeleka katika kituo cha Polisi Magomeni huku
polisi hao wakiwazuia waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao na maandamano ya vijana hao yaliishia hapo.
Kiukweli wameweke Record ya mwaka2015
ReplyDeleteWameonyesha uzalendo tatizo wa tz wengi sasa hivi wabinafsi hasa walio na uhakika wa maisha wanawabeza sana wapigania usawa lakini kitaeleweka 2 mungu wa wote wala sio mjomba wa mtu
ReplyDelete